Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 12:57

Mfalme Charles na Camilla watazama mafunzo Kenya yaliyotolewa na jeshi la maji la Uingereza


Mfalme Charles akikagua jeshi lililoandaliwa kwa heshima yake alipowasili Mombasa Novemba 2, 2023. Picha na Ian Vogler / POOL / AFP.
Mfalme Charles akikagua jeshi lililoandaliwa kwa heshima yake alipowasili Mombasa Novemba 2, 2023. Picha na Ian Vogler / POOL / AFP.

Mfalme Charles na Malkia Camilla Alhamisi aliwatazama wanamaji wa Kenya walichukua mafunzo kutoka kwa wananaji wa Uingereza wakitua kwenye ufuo wa bahari katika siku ya tatu ya ziara yao rasmi katika koloni la zamani la Uingereza.

Baada ya siku mbili katika mji mkuu Nairobi, Charles na Camilla alisafiri hadi katika mji wa bandari wa Mombasa, ambao ulikuwa mji mkuu wa awali wa British East Africa.

Zoezi la mafunzo hayo , ambayo kilishuhudia jeshi la wanamaji wakiwa ufukweni wakielekea uliko msafara wa kifalme huku mabomu yalitoa moshi mwekundu yakizunguka juu, ilikiamanisha uwepo wa uhusiano wa karibu wa ulinzi kati ya Uingereza na Kenya.

Ziara ya kwanza ya Charles katika koloni la zamani tangu alipotwaa kiti cha enzi mwezi Septemba mwaka jana, imekuwa na maswali kuhusu dhuluma wakati wa utawala wa Muingereza wa takribani miongo saba nchini humo.

Wakati wa uasi wa Mau Mau mwaka 1952-1960 katika eneo la katikati mwa Kenya, baadhi Wakenya 90,000 waliuawa au kulemazwa na 160,000 waliwekwa vizuizini, Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KHRC) imekadiria.

Mfalme Charles akiwa ameketi ufukweni mwa bahari pamoja na wazee wa eneo la hifadhi ya Kuruwitu iliyoko Kilifi Novemba 2, 2023. Picha na PHIL NOBLE / POOL / AFP.
Mfalme Charles akiwa ameketi ufukweni mwa bahari pamoja na wazee wa eneo la hifadhi ya Kuruwitu iliyoko Kilifi Novemba 2, 2023. Picha na PHIL NOBLE / POOL / AFP.

Jeshi la Uingereza pia linakabiliwa na uchunguzi wa kina wakati wa ziara ya Charles. Siku ya Jumatatu, polisi wa Kenya walizuia mkutano wa wanahabari iliyokusudiwa kurusha habari kuhusiana na madai ya dhuluma zilizofanywa na kitengo cha kambi ya mafunzo ya jeshi la Uingereza kilichoko eneo la katikati mwa Kenya.

Wakaazi wamewashutumu wanajeshi wa Uingereza kwa kusababisha a moto wa mwituni mwaka 2021 ambao uliharibu sehemu kubwa ya hifadhi ya asili, na kusababisha majeraha kwa wakazi wa eneo hilo, na kudai walihusika katika mauaji ya mwaka 2012 ya mwanamke aliyeonekana mara ya mwisho na a askari wa Uingereza.

Mamlaka ya Uingereza iliahidi katika siku za nyuma kuchunguza tuhuma dhidi ya wanachama wa kitengo hicho cha mafunzo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG