Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 13, 2024 Local time: 06:18

Marekani yaitaka Israel kuhakikisha Wapalestina wanalindwa na wanapata msaada wa chakula


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumatano alisema kwamba Israel yapaswa kuzingatia usalama wa raia wa Palestina kama kipaumbele cha kwanza katika vita vyake dhidi ya Hamas huko Gaza.

“Tunatarajia kuwa serikali ya Israel itahakikisha hili kama kipaumbele. Kulinda raia, kuruhusu watu kupata msaada wanaouhitaji,” aliwambia waandishi wa habari baada ya mkutano na washirika wa kimataifa kwa njia ya mtandao.

“Hili lapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza, hata kama wanafanya kile kinachohitajika kuilinda nchi na kukabiliana na tishio la Hamas.”

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani alikutana kwa njia ya video na mawaziri wa Cyprus, Uingereza, Umoja wa falme za kiarabu, Qatar, Umoja wa Ulaya na Umoja wa mataifa kujadili njia mpya ya baharini kusafirisha msaada hadi Gaza. Jeshi la Marekani lilipeleka meli kwenye Bahari ya Mediterranean kujenga daraja la muda kwenye ufukwe wa Gaza kufungua njia kwa malori zaidi ya misaada lakini linasema ujenzi huo utachukua miezi kadhaa ili kukamilika.

Forum

XS
SM
MD
LG