Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 11:12

Marekani inataka kikosi cha RSF kuacha kushambulia raia

Bendera ya Sudan iliyowekwa kwenye mtuta wa bunduki ya kikosi cha kijeshi cha RSF wakati wapiganaji walikuwa wanamlinda kamanda wao Lt Gen. Mohamed Hamdan Dagalo kabla ya mkutano mjini Aprag, kilomita 60 kutoka Khartoum. June 22, 2019

Marekani imetoa wito kwa kikosi cha kijeshi cha Sudan kuacha kushambulia maeneo ya raia, ikisema kwamba hatua hiyo inaendelea kuwaweka watu wa Sudan katika mateso makubwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema katika taarifa kwamba kikosi cha kijeshi cha RSF kinastahili kuacha kupiga makao ya raia na badala yake kuwalinda raia hao katika sehemu za Nyala, Omdurman na kote Sudan.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, wapiganaji wa RSF wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa Sudan tangu mwezi Aprili katika vita ambavyo vimepelekea vifo vya zaidi ya watu 5000 na kupelekea zaidi ya watu milioni 5 kukoseshwa makazi.

Wapiganaji wa RSF wameongeza mashambulizi katika sehemu za Omdurman zinazoshikiliwa na wanajeshi wa serikali. Kundi hilo lia limeendelea kutekeleza mashambulizi kwenye kambi za kijeshi katika sehemu za Nyala, magharibi mwa Darfur, wakiwa na lengo la kuudhibithi mji huo.

Forum

XS
SM
MD
LG