Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 07:09

Marekani inaitaka Syria kusitisha ghasia dhidi ya raia


Wandamanaji wakihudhuria maziko ya wenzao walouliwa na vikosi vya usalama huko Syria.
Wandamanaji wakihudhuria maziko ya wenzao walouliwa na vikosi vya usalama huko Syria.

Kwa mara ya kwanza White House imetoa kauli inayoleza kwamba miongoni mwa mambo rais anatafakari ni kuiwekea Syria vikwazo.

Serikali ya Marekani inaongeza shinikizo kwa serikali ya Syria kusitisha utumiaji nguvu katika kukabiliana na waandamanaji.

Kwa mwezi mmoja uliopita, ikulu ya Marekani imeshatowa taarifa tano kuhusu vurugu huko Syria, iwe ni ujumbe wa moja kwa moja kutoka kwa Rais Barack Obama au kupitia kwa msemaji wa rais, au Baraza la Usalama wa Taifa NSC.

Ujumbe wa mwisho ulitoka Jumatatu kwa njia ya barua pepe kutoka kwa msemaji wa NSC Tommy Vietor. Ameeleza ghasia za serikali ya Syria dhidi ya watu wake kuwa ni “jambo la kulaaniwa ” na kwamba Marekani inatafuta njia zote za kisiasa inazoweza kutumia kusitisha hili.

Vietor amesema kwamba hatua zinazofikiriwa zinaweza kuhusisha vikwazo maalum ili “kuweka bayana kwamba tabia hii haikubaliki.”

Ameongeza kusema kwamba “wito wa watu wa Syria wa kuwa na uhuru wa kujieleza, kuweza kukusanyika kwa amani, na uwezo wa kujichagulia viongozi wao kwa uhuru ni lazima usikilizwe.”

XS
SM
MD
LG