Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 12:36

Mapinduzi ya nchi za Kiarabu 2011


Malefu ya waandamanaji wa Bahrain
Malefu ya waandamanaji wa Bahrain

Mwaka 2011 utakumbukwa kuwa mwaka wa mapinduzi makubwa duniani yaliyoanza Afrika ya Kaskazini.

Nani aliyetarajia kujitia moto kijana wa ki-Tunisa Mohamed Bouazizi hapo Disemba 17 2010 na kufariki Januari 7, kungezindua upinzani wa wananchi hadi mapinduzi katika baadhi ya nchi za kiarabu. Mapinduzi yalishuhudia kuondolewa kwa viongozi watatu wa muda mrefu wa Afrika Kaskazini, rais Zein Al Abidine Ben Ali wa Tunisia aliyetoroka Januari 14, akifuiatiwa na kujiuzulu kwa rais Hosni Mubarak Februari 11 na kuondolewa na kuuliwa kwa Moammar Gadhafi Oktoba 20.

Dr Bashiru Ally mhadhir wa chuo kikuu cha Dar es Saalam, anasema inategemea jinsi unavyo tizama mapinduzi hayo.

inategemea mtu anavyosema watu wengine wanasema nchi za kiarabu sasa ndio zinaanza kupitia mpito wa kufanya maboresho ya mifumo yao ya kisiasa na kupanua uhuru wa wananchi kudhibiti serikali zao. Kwa hiyo huo ni mtazamo ambao wengine wanaona ni mtazamo mzuri.”

Kwa miongo kadhaa maisha ya watu walio wengi katika kanda hiyo yalikuwa yamebaki pale pale. Watu wachache wakisaidiwa na tawala za kimabavu waliweza kutajirika na familia zao kuendesha biashara za mataifa hayo.

Ile hali ambayo hakuna aliyedhani itabadilika basi ilibadilika pale vijana waliamua hawarudi tena nyuma dhidi ya watawala wakimabavu, anasema Heba Morayef wa kundi la Human Rights Watch.

“Moja wapo ya matukio tuloshuhudia katika mataifa mengi yaliyokuwa na mapinduzi yaliyopewa jina la Arab spring, kwanza Tunisia, halafu misri, ikifuata Libya na Syria ni picha kawaida za vijana wanaume ambao wako tayari kukufaa kwa ajili ya misingi ya uhuru, misingi ya haki. Mbele ya maafisa wa usalama wenye bunduki mji mmoja baada ya mwengine na ushujaa huu mpya wa kusimama wima dhidi ya unyanyasaji tiloshuhudia kwa hjakika ndio kilicho chochea Arab Spring.”

Mhadhir wa chuo kikuu cha Al Azhar Ismael Mfaoume anasema ni mwaka wa kukumbukwa na mwaka wa mageuzi makubwa na yeye anataja pia matukio ya huko Sudan

“Mimi nina anzia mbali kidogo, nina anzia na Sudan. Kupatikana kwa taifa jipya la kusini mwa Sudan, yani Sudan kugawanyika kuwa Sudan mbili. Hilo lilikua miongoni mwa matukio muhimu sana ya mwaka unaomalizika. Halafu vile vile mapinduzi yaliyoendeshwa na wananchiwa kawaida ambao sio jeshi wala si chechote katika kama nchi tano za Kiarabu, lakini tatu tayari zimefanikiwa. Ikiwa ni kuanzia Tunisia, Misri na Libya. Na nchi mbili wananchi baado wanaendelea kupambana na viongozi wao ili wan’gatuke madarakani, yani Syria na Yemen.”

Nae Heba wa Human Rights Watch anasema upinzani huu wa wananchi haujabadilisha tu watawala wa mataifa haya bali pia kuvuruga ushirika wa muda mrefu.

“Kwa mtizamo huo imepelekea hali ya kutoweza kutabiri Mashariki ya Kati kanda iliyochukuliwa tulivu, watawala wa kimabavu kuwakabidhi mara nyingi madaraka watoto wao na ambako Jumuia ya Kimataifa iliweza kutegemea kuwa na baadhi ya marafiki katika kanda ambao walihakikisha uthabiti. Ninadhani mitizamo hiyo ya Mashariki ya Kati imevurugika”.

Huko Saudi Arabia taifa kuu la kifalme wananchi walijaribu kujitokeza lakini juhudi kuzimwa haraka ingawa kumetokea mabadiliko kama vile mwandishi habari Abdallah Wachu akiwa Riadha anavyoeleza.

“Kwa upande wa Saudia kama inavyojulikana kwamba hapa serikali hairuhusu au hakuna ile demokrasia inashuhudiwa katika maeneo mengine kwa sababu utawala wenyewe kwanza kabisa ni wa kifalme. Na hakuna uchaguzi kama vile uchaguzi wa bunge, wa rais, na vitu kama hivyo, kwa hivyo hakuna mabadiliko makubwa ambayo yameshuhudiwa hapa.”

Mara baada ya upinzani wa Misri wakazi walowengi wa Bahrani wa dhehebu la Shia waliandamana kutaka mageuzi na mapinduzi yao kujulikana kama mapinduzi ya “Februari 14”. Bw Wachu anasema,

“Wananchi wengi asili mia kubwa ya wananchi nchini Bahrani ni wa jamii ya madhehebu ya Shia na utawala unaotawala nchini humo ni wa dhehebu la Suni. Kwa hivyo wananchi pale wanalalamika kwamba utawala huo una wanyanyasa una kandamiza haki zao za kidemokrasia na kijamii. Kwa hivyo walianzisha harakati za kutaka kuhakikisha wanapata haki zao za kimsingi na wala si kupindua serikali.

Upinzani wa wananchi wa Bahrain ulizimwa kutokana na msaada wa nchi jirani wa Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ambapo majeshi ya Saudia yalipelekwa March 14 na siku ya pili mfalme Hamad bin Issa bin Khalifa, alitangaza utawala wa kijeshi na hali ya utawala wa dharura kwa miezi mitatu.

Hapo tena pakazuka upinzani mkubwa Yemen na Syria ambao umendelea hadi mwisho wa mwaka. Nchini Yemen Ali Saleh alikubali hatimae kuacha madaraka mwezi Disemba na kuruhusiwa kusafiri hadi Marekani kwa ajili ya matibabu.

Lakini jambo kuu katika mapinduzi hayo yote ni vijana wa nchi hizo, anasema Mfaoume.

“Jukumu lao ni kubwa na vile vile mabadiliko haya ambayo ya hapa Misri huwa wanaita kwamba ni mabadiliko au mapinduzi ya internet. Ni kwamba vijana wamethibitisha uwezo wa kutumia vyombo vya kisasa na kuweza kuwasiliana na kupanga kwa utaratibu ulomzuri na kufanikiwa mapinduzi yao. Na vijana wengi hapa Misri wanafuraha kubwa sana kwamba pengine haya mapinduzi yatapelekea kupatikana mabadiliko makubwa sana.”

Wanawake pia walikua na jukumu kubwa katika mapinduzi hayo ya nchi za kiarabu ambapo Tawwakul Karaman mwanamke mwenye umri wa miaka 32 wa Yemen alipokea tunzo ya Amani ya Nobel pamoja na rais wa Liberia Bi Ellen Johnson Sirleaf na Leyhman Gbowe, kutokana na kampeni zake za kupigania haki za binadam na kusimama kwenyue uwanja mkuu wa Sanaa tangu upinzani kuanza sawa na yale ya misri.

Mmoja kati ya sababu kuu ya kuzuka upinzani huo katika nchi za kiarabu unaotokana na uwongozi na Dr Bashiru Ally anasema.

“Mimi ninadhani suala la kutawala muda mrefuau kutawala muda mfupi kwa kiongozi, halina nafasi kubwa sana kwa kuelezea tatizo linaloikabili dunia na uwongozi kwa ujumla wa kisiasa. Kiongozi anaweza akatawala kwa muda mnfupi sana nab ado akawa mtu hatari. Hitler hakutawala miaka mingi. Hitler alitawala kwa muda mrefu,lakini muda huo ulileta maafa makubwa kwa Wajerumani na kwa dunia.”

Na somo kubwa linalotokana na Arab Spring au mapinduzi ya nchi za kiarabu ni kwamba chechote kinaweza kutendeka na hata wananchi wa kawaida wanauwezo wa kuleta mabadiliko

Nae Dk. Bashiru Ally, wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anasema licha ya matokeo hayo haijulikani wazi muelekeo utakua upi huko Mashariki ya Kati.

“Kwa muda mrefu hizo serikali za mataifa ya Kiarabu zimekuwa na matatizo ya ndani ya namna ya kutawala, hakuna mfumo wa wazi na ulio wa kidemokrasia wa kubadilisha mamlaka na madaraka na kuweka misingi ya utawala ambao unalinda haki za walio wengi.”

Upinzani huo wote wa wananchi wa 2011 ulitokea katika takriban katika kila nchi ya kiarabu lakini kuna baadhi ya viongozi walotumia busara kubwa na kukubali kufanya mageuzi ya haraka ya katiba au utawala kamaalivyo fanya mfalme Mohamed wa Moroco na Abdullah wa Jordan.

Na tukio moja muhimu ambalo halikudumu sana kwenye vichwa vya habari ni kuuliwa kwa Osama bin Laden na Anwar al-Awlaki huko Yemen na hivyo kuvunja nguvu sana makundi yenye siasa kali ya kislamu hasa Al Qaida.

Na mapinduzi ya muamko wa nchi za kiarabu yalipelekea mageuzi makubwa Misri, Tunisia na Libya ambako uchaguzi uliweza kufanyika kwa amani huko Tunisia na wanaandika katiba mpya, Misri uchaguzi unamalizika kuchagua bunge na Libya serikali ya mpito inajitayarisha kuitisha uchaguzi wake.

Na mapinduzi haya ya vijana yameleta matumaini na kufungua ukurasa mpya wa nyimbo za mapinduzi.

XS
SM
MD
LG