Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 07:30

Huenda wanasiasa wanatumia makundi ya kigaidi Kenya-Wachambuzi


Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.
Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.

Taarifa za kuuawa kwa wakenya kumi na wawili katika shambulizi la kuamkia Jumanne katika hoteli ya Bishaaro katika mji wa Mandera zimewaacha wengi kinywa wazi nchini humo wasifahamu ni kwa nini mashambulizi ya aina hii yamekuwa yakifuatana kwa ukaribu mno.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:48 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Ni kutokana na tukio hili ambapo Rais Uhuru Kenyatta amekatiza ghafla ziara yake rasmi jijini Luanda nchini Angola ili kuzifariji familia ambazo zimeathirika na shambulizi hilo. Katika taarifa kwa vyombo vya habari Rais Kenyatta amesema,"Kenya haitakubali kugawanywa kwa misingi ya kidini, ambalo ni jambo ambalo magaidi wanalitafuta,” .

Rais Kenyatta kando na kulaani vikali shambulizi hilo amewataka wakenya kushirikiana kwa ukaribu mno na vyombo vya usalama kukomesha mianya inayotumiwa na magaidi.

Mapema mwezi huu, watu sita walipoteza maisha yao katika eneo la Bulla mjini Mandera na kuzidisha idadi ya wakenya ambao wamefariki mikononi mwa wanamgambo wa Alshabaab. Hata baada ya serikali ya Kenya kuongeza juhudi nyingi za kuzima nguvu za magaidi hawa, visa hivi vimekuwa vikiongezeka wiki baada ya wiki.

Kile ambacho pia kinapigiwa darubini ni jinsi wanamgambo hawa wameanza kushambulia migahawa,majengo na makazi ya watu mjini Mandera kinyume na ilivyokuwa ada walipokuwa wakivishambulia vituo vya polisi.

Hilo kando, wenyeji wanaripotiwa kushirikiana na wanamgambo hao kutekeleza mashambulizi hayo. George Musamali mchambuzi wa masuala ya usalama anaeleza kuwa kushirikiana kwa wenyeji na wanamgambo hao huenda wakaleta udhaifu kwa juhudi za serikali kukabiliana vilivyo na tishio la ugaidi nchini.

Serikali ya Kenya imekuwa mbioni kuzima mafunzo ya itikadi kali kudhibiti mianya yoyote itakayolipa kundi hilo haramu nafasi ya kuwaangamiza wananchi.

Bwana Musamali anaeleza kuwa huenda ikawa wanasiasa wa ukanda huo wanatumia makundi ya kigaidi kuangamizana kisiasa na kibiashara.


XS
SM
MD
LG