Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 12:02

Mshindi wa Nobel Malala Yousafzai atembelea wakimbizi Daadab


 Malala Yousafzai (kushoto) akiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Daadab Jumanne.
Malala Yousafzai (kushoto) akiwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Daadab Jumanne.

Mshindi wa Nobel Malala Yousafzai atembelea wakimbizi Daadab wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwake ya kumi na saba.

Mshindi wa tuzo la Nobel kutoka Pakistan Malala Yousafzai alisherehekea mwaka wake wa 17 tangu kuzaliwa Jumanne, akiwa kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi ulimwenguni na ambayo serikali ya Kenya inanuia kufunga kufikia mwisho wa mwaka ya Daadab.

Zaidi ya wakimbizi 300,000 wengi wao kutoka Somalia huita kambi hiyo ilioko mashariki mwa Kenya nyumbani . Serikali ya Kenya imedai kuwa mashambulizi yanayofanywa nchini na kundi la Al-shabab huwa yanapangiwa kwenye kambi hiyo na kwa hivyo kusema ni tishio la usalama taifa.

Malala alisema kuwa hakuna yeyote anaestahili kulazimishwa kurudi Somalia hasa wasichana ambao tumaini lao la masomo ni shule za Umoja wa Mataifa zilizoko kwenye kambi hiyo. Ameongeza kusema bila masomo, hatma ya wasichana hao itakuwa ndoa za mapema na maisha yao yatakuwa yamefika kikomo.

XS
SM
MD
LG