Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 07:38

Liberia yaanzisha mahakama ya uhalifu wa kivita


Rais wa Liberia Joseph Nyumah Boakai
Rais wa Liberia Joseph Nyumah Boakai

Rais wa Liberia Joseph Boakai siku ya Alhamisi alitia saini amri ya kiutendaji ya kuanzisha mahakama ya uhalifu wa kivita yenye lengo la kuleta haki kwa waathiriwa wa dhuluma kubwa zilizofanywa wakati wa vita viwili vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Wachambuzi wanasema hatua hiyo ilikuwa imechelewa.

Vita vya ndani kati ya 1989 na 2003 ilishuhudia ukatili mkubwa ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, na matumizi ya askari watoto.

Baadaye Kamati ya Ukweli na Maridhiano iliitaka mahakama maalum iundwe kuwasikiliza wanaodaiwa kuhusika.

Hata hivyo, hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa hadi Boakai alipochaguliwa mwaka jana. Rais huyo alipendekeza azimio la kuunda mahakama maalum, ambalo baadaye liliungwa mkono na bunge la chini la Liberia na seneti.

Siku ya Alhamisi, Boakai aliwashukuru wabunge kwa kazi yao na akatoa idhini yake ya mwisho.

Forum

XS
SM
MD
LG