Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 02:58

Kiongozi wa bunge la Vietnam ajiuzulu


Mwenyekiti wa bunge la Vietnam, Vuong Dinh Hue amejiuzulu kutokana na ukiukwaji wa masuala kadhaa serikali yake imesema Ijumaa, ikiwa ni ishara mpya ya msukosuko wa kisiasa wiki chache tu baada ya kufutwa kazi kiongozi wa ngazi ya juu yaani rais wa nchi hiyo.

Mkuu wa bunge ni miongoni mwa nguzo nne muhimu za uongozi kwa Vietnam, ambayo rasmi sasa haina kiongozi mkuu.

Hue, mwenye umri wa miaka 67, amekuwa amepigiwa debe kuwa mgombeaji wa nafasi ya katibu wa Chama cha Kikomunisti, kazi yenye nguvu zaidi Vietnam.

“Ukiukwaji wa masuala na matokeo yake wa Komredi Vuong Dinh Hue, umesababisha maoni mabaya kutoka kwa umma, na kuathiri sifa za Chama, taifa na yeye binafsi,” tovuti ya serikali imeandika, ikiwa na taarifa kutoka kwa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti.

Forum

XS
SM
MD
LG