Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 16, 2024 Local time: 22:28

Kifo cha mshukiwa wa mauaji ya 1994 Rwanda, kimechukiza manusura


Kundi la walio nusurika mauaji ya kimbari ya Rwanda, Jumapili lilionyesha kukasirishwa kutokana na Laurent Bucyibaruta, afisa wa zamani aliyepatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya 1994, kufariki dunia wiki hii bila kukabiliwa na sheria.

Bucyibaruta, ambaye alifariki Jumatano akiwa na umri wa miaka 79, alikuwa Mnyarwanda wa cheo cha juu zaidi aliyekabiliwa na kesi nchini Ufaransa kutokana na mauaji ya mwaka 1994 ambapo takriban Watutsi, 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuwawa katika siku 100 za mauaji ya kimbari.

Bucyibaruta alipatikana na hatia Julai 2022, ya kushiriki mauaji na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mkoa wa kusini wa Gikongoro, na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20.

Akiwa mmoja wa Wanyarwanda wachache waliofikishwa mahakamani nchini Ufaransa, alikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na kuachiliwa kutoka gerezani akisubiri kesi mpya mpaka umauti ulipomkuta.

Forum

XS
SM
MD
LG