Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 07:54

Kenyatta aomboleza kifo cha Nabhany


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwanazuoni wa Kiswahili na Mshairi maarufu duniani, Prof Sheikh Ahmed Mohamed Nabhany, aliyeaga dunia Alhamisi asubuhi.

Kenyatta ametoa wasifu wa mwanazuoni huyo kwa kusema kuwa alichangia kwa kiwango kikubwa katika tafiti za lugha ya Kiswahili nchini Kenya na nje ya nchi, vyanzo vya habari vimesema.

“Sisi tutaendelea kumuenzi Marehemu Nabhany katika maandishi yake na kufundisha kwake lugha ya Kiswahili, mashairi na utamaduni ambazo zilipata umaarufu dunia nzima,” Rais Kenyatta amesema.

Rais ameongeza kuwa kifo cha mwanazuoni huyu wa kipekee kimeacha mwanya mkubwa ambao ni tabu kuuziba.

“Katika kipindi hiki cha huzuni na masikitiko, fikra zangu na dua zangu nazielekeza kwa familia ya marehemu, ndugu na marafiki. Ni maombi yangu Mwenyezi Mungu Mtukufu awapeni nguvu katika kusubiri,” Kenyatta amesema.

Mwanzuoni huyu maarufu alikuwa amejielimisha yeye mwenyewe lakini aliweza baadae katika uhai wake kufundisha Kiswahili katika vyuo vikuu vikiwemo vile vya Ulaya.

“Mimi sijawahi kupata fursa wakati wa utoto wangu kwenda shuleni lakini niliweza kujielimisha mwenyewe hapa Mombasa,” alisema hayo Profesa katika mahojiano yake ya siku za nyuma.

Sheikh Nabhany amezikwa siku ya Alhamisi jioni katika makaburi ya Matondoni huko katika kaunti ya Lamu.

XS
SM
MD
LG