Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 01:02

Kenya yaondoa vikosi vyake Sudan Kusini


Wanajeshi wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Matiafa Sudan Kusini.
Wanajeshi wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Matiafa Sudan Kusini.

Serikali ya Kenya Jumatano imepinga vikali hatua ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumuondoa Luteni Jenerali Johnson Mogoa Kimani Ondieki kama kamanda wa kikosi cha kulinda usalama Sudan Kusini.

Serikali ya Kenya siku ya Jumatano ilipinga vikali hatua ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumuondoa Luteni Jenerali Johnson Mogoa Kimani Ondieki wa Kenya kama kamanda wa kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS).

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Kenya, ilisema kutokana na hatua hiyo ambayo wanaiona haikufuata taratibu sahihi, imeamua haraka kuondoa wanajeshi wa Kenya ambao hivi sasa wapo nchini Sudan Kusini na kutoendelea na mipango ya kuchangia katika kikosi cha kieneo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo serikali ya Kenya ilijulishwa kuondolewa kwa Luteni Jenerali Ondieki na hivyo kutakiwa kutafuta mtu atakayechukua nafasi yake, jambo ambalo serikali ya Kenya inaamini kwamba Umoja wa Mataifa na tume maalum ya uchunguzi hawakulishughulikia vyema suala hilo kwa kuangalia kiini cha tatizo kwa matukio mbali mbali ambayo yamejitokeza nchini Sudan Kusini.

Kutokana na kutoridhishwa na hatua hiyo serikali ya Kenya imesema pia inajitoa katika kujihusisha na utaratibu wa Amani wa Sudan Kusini.

Taarifa imeendelea kusema kuwa utaratibu huo ulikuwa hauna uwazi na haukuhusisha mashauriano yoyote rasmi na serikali ya Kenya. Na hili linaonyesha wazi kutotilia maanani jukumu na wajibu wa vikosi vya Kenya nchini Sudan Kusini.

XS
SM
MD
LG