Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:50

Kazi iliyofanywa na mataifa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa haitakuwa ya bure-John Kerry.


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akitoa maelezo huko Marrakech, Morocco, Nov. 16, 2016.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akitoa maelezo huko Marrakech, Morocco, Nov. 16, 2016.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, amesema kwamba kazi iliyofanywa na mataifa ya ulimwengu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, haitakuwa ya bure pale rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump, atakapochukua hatamu za uongozi, kwa sababu ameyaita mabadiliko hayo kama utani.

Kerry ameambia mkutano wa Umoja wa mataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa mjini Marakesh, Morocco, kwamba ana imani kuwa makubaliano yaliyoafikiwa mjini Paris kuhusiana na swala hilo, yataendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa, kwa sababu maamuzi hayatoki kwa serikali za nchi binafsi.

Kerry alisisitiza umuhimu wa kutekeleza makubaliano hayo ya Paris, na kusema kuwa itakuwa hatua ya kihistoria na ambayo inawapa watu wengi matumaini. Trump, ambaye alichaguliwa kama rais wilki iliyopita, ameahidi kufutilia mbali ushirika wa Marekani katika makubaliano hayo ya mwaka jana, ambayo yalipelekea kukubali kwamba nchi mia mbili kupunguza utoaji wa hewa chafu.

Makubaliano hayo ya Paris yalianza kutekelezwa mwezi huu, baada ya idadi ya nchi zilizoratibu kuongezeka na kufikia kiwango kilichohitajika.

XS
SM
MD
LG