Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 09:51

Jimbo la Florida lapitisha sheria mpya inayopiga marufuku utoaji mimba


Makamu wa Rais Kamala Harris anazungumza juu ya utekelezaji wa marufuku ya utoaji mimba huko Florida Jumatano, Mei 1, 2024, huko Jacksonville, Florida.
Makamu wa Rais Kamala Harris anazungumza juu ya utekelezaji wa marufuku ya utoaji mimba huko Florida Jumatano, Mei 1, 2024, huko Jacksonville, Florida.

Jimbo la Florida, Marekani, limepitisha sheria mpya inayopiga marufuku utoaji mimba baada ya wiki sita za ujauzito.

Kampeni ya Biden inafanya haki ya uzazi kuwa kipaumbele cha harakati zake, za kuchaguliwa tena. Makamu wa Rais Kamala Harris alifanya kampeni katika jimbo la Florida katika siku ambayo sheria mpya ya utoaji mimba ilianza kutekelezwa.

Sheria mpya ya utoaji mimba ya Florida ni miongoni mwa sheria kali zaidi nchini, na imesababisha shinikizo la suala la haki za utoaji mimba kuwekwa kwenye katiba, kupitia uchaguzi wa mwezi Novemba.

Majimbo ya Marekani yanatunga sheria zao kuhusu mimba kwa sababu uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2022, ulikomesha udhibiti wa seriakli kuu kuhusu suala hilo.

Trump aliteua majaji watatu kati ya sita walioamua kesi hiyo, na Harris anasema wapiga kura wanahitaji kumuwajibisha.

Ingawa Trump anasema sheria mpya ya Florida inavuka mpaka, mara kwa mara anapokea sifa kuhusu uamuzi wa mahakama ya juu, ulioyapatia majimbo uhuru wa kuamua “Ni mapenzi ya watu" alielezea kwenye video kwenye kupitia mtandao wake wa kijamii mwezi uliopita.

Mmiliki wa kliniki Candace Dye anasema kulikuwa na msongamano wa wagonjwa kabla ya sheria mpya ya utoaji mimba. Kwake, marufuku ya wiki sita ni adhabu kali zaidi.

Nje ya kliniki, waandamanaji wanaopinga utoaji mimba hujaribu kuwasilian na kila mwanamke anayeingia. Tammy Holly anatoa maoni yake.

Wakati kukomesha utoaji mimba kukiwapa motisha wapiga kura wengi wa Republican, Trump anaonekana kulichukulia suiala hilo kwa uangalifu wa kisiasa katika kinyang'anyiro cha urais chenye ushindani mkubwa.

Harris anasema washirika wa Trump wa chama cha Republican katika Bunge wanataka marufuku ya utoaji mimba itekelezwe nchini kote.

Trump amesema hilo si jambo la lazima kwa sasa, kwamba majimbo yanaweza kujitengenezea sheria za utoaji mimba.

Forum

​
XS
SM
MD
LG