Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 12:19

Israeli imeishambulia Iran - Maafisa wa Marekani


PICHA YA MAKTABA: Mfumo wa ulinzi wa anga dhidi ya makombora wa Iran.
PICHA YA MAKTABA: Mfumo wa ulinzi wa anga dhidi ya makombora wa Iran.

Israeli ilifanya shambulizi la kombora Ijumaa alfajiri ndani ya Iran, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti, vikiwanukuu maafisa wa utawala wa Biden ambao hawakutajwa majina.

Ripoti za mashirika ya habari ya ABC, CBS na NPR hazikutoa maelezo zaidi kuhusu eneo au lengo la shambulio hilo la kombora.

Msemaji wa jeshi la Israel aliiambia VOA kuwa hana maoni yoyote "kwa sasa" kuhusu ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, takriban saa moja baada ya ripoti hizo kutokea.

Shirika la habari la serikali ya Iran IRNA limesema ulinzi wa anga wa jamhuri ya Kiislamu umeanzishwa angani katika majimbo kadhaa.

IRNA na shirika la habari la serikali Fars, lenye mafungamano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, walinukuu vyanzo vya habari ambavyo havikutajwa vikisema "kumetokea mlipuko katika mkoa wa kati wa Iran wa Isfahan."

Fars walipata mlipuko huo katika mji wa Qahjaverestan, viunga vya mashariki mwa mji wa Isfahan.

Israel ilikuwa imeionya Iran kwamba italipiza kisasi kwa shambulio la anga la Iran ambalo halijawahi kushuhudiwa dhidi ya Israel Jumapili iliyopita.

Iran ilikuwa imeonya, kwa upande wake, kwamba hatua yoyote ya kulipiza kisasi ya Israel ingekabiliwa na jibu la haraka na kali zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG