Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 19:26

Israel haijasema lolote kuhusu mashambulizi ndani ya Iran


Watu wakifanya mgomo dhidi ya Israel kwenye mji mkuu, Tehran. Aprili 19, 2024
Watu wakifanya mgomo dhidi ya Israel kwenye mji mkuu, Tehran. Aprili 19, 2024

Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa Israel imefanya mashambulizi ya anga nyakati za alfajiri ndani ya Iran Ijumaa vikiwanukuu maafisa wa Israel na Marekani ambao hawakutajwa majina.

Magazeti ya The New York Times na Washington Post yamewanukuu maafisa hao wakisema kuwa Israel imefanya shambulizi la anga ndani ya Iran, wakati maafisa kadhaa wa Marekani waliotajwa na vyombo kadhaa vya habari wakisema kuwa lilikuwa shambulizi la kombora.

Hata hivyo mpaka sasa eneo lililoshambuliwa halijatajwa. Baada ya takriban muda wa saa moja kufuatia ripoti hizo, msemaji wa jeshi wa Israel aliyezungumza na VOA alisema kuwa hakuna lolote la kusema kuhusiana na tukio hilo.

Mashirika ya habari ya Iran yanalomilikiwa na serikali ya IRNA na Fars yamesema kuwa mfumo wa ulinzi wa anga wa taifa hilo la kiislamu umeanza kufanyishwa kazi kwenye mji wa kati wa Isfahan, kufuatia shambulizi hilo la Israel.

Mashirika hayo pia yamesema kuwa milipuko ilisikika kwenye vitongoji vya mashariki mwa mji huo, bila kufafanua iwapo ilikuwa ni kutokana na kunaswa kwa silaha zilizorushwa, au milio ya pale zilipotua ardhini. Mratibu wa idara ya anga za juu wa Iran amesema kuwa jeshi la anga limeangusha droni kadhaa zilizorushwa na Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG