Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 00:08

Waziri mkuu wa India Narendra Modi ahutubia bunge la Marekani


Waziri mkuu wa India Narendra Modi akihutubia bunge la Marekani
Waziri mkuu wa India Narendra Modi akihutubia bunge la Marekani

Kama kiongozi wa taifa liillokumbwa na migawanyiko ya madhehebu, kidini na kikabila, waziri mkuu wa India Narendra Modi anatafuta uwelewano na wabunge wa marekani kwa kutumia ucheshi.

Bw Modi aliwaambia wabunge wa Marekani kuwa nimeambiwa kazi ndani ya bunnge zinafanyika kwa Amani. Anasema pia nimeambiwa kuwa mnajulikana sana kwa ushirikiano baina ya vyama vyenu. Bw Modi alipigiwa makofi ikifuatiwa na vicheko baada ya kutoa kauli hiyo, pale alipokutana na wabunge wa Marekani jana Jumatano.

Bw Modi aliendelea kuwaambia wabunge hao kuwa hawako peke yao. Alisema, mara kwa mara yeye pia hushuhudia hali kama hiyo katika bunge la India. Kwa hivyo tuna mifano mingi ya pamoja.

Bw Modi alisema kushamiri kwa ushirikiano wa biashara na nishati, na hata maslahi ya kimkakati, na kuongezea kuwa umbali na hali ya kutokuaminiana amabyo awali iliashiria uhusiano wa India na Marekani, sasa ni jambo la zamani.

Anasema uhusiano wetu umevuka kusitasita za historia, na sasa ukweli na muunganiko unafafanua majadiliano yetu, na bw Modi alisihi kuwepo na ushirikiano wa karibu zaidi kwa malengo yao pamoja.

Hotuba ya Modi ilikuwa ni ya tano kuwahi kutolewa na mkuu wa serikali ya India kwa bunge la marekani. Hotuba hio inafwatia mkutano wa jumanne na rais Barack Obama na tangazo kuwa India itajenga vinu 6 vya nyuklia vitakavyojengwa na makampuni ya Marekani, hiyo ikiwa matokeo ya makubaliano ya kiraia ya kinyuklia kati ya mataifa hayo mawili ambayo yalifikiwa mwaka 2008.

XS
SM
MD
LG