Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 10:48

Gaza: Israel yaapa kukivunja kabisa kikundi cha wanamgambo wa Hamas

Wanajeshi wa Israeli wakiyasogeza magari ya kivita na kukusanyika katika mpaka wa Ukanda wa Gaza October 16, 2023, huku mapigano yakiendelea kati ya Israel na kikundi cha Palestina cha Hamas.
Wanajeshi wa Israeli wakiyasogeza magari ya kivita na kukusanyika katika mpaka wa Ukanda wa Gaza October 16, 2023, huku mapigano yakiendelea kati ya Israel na kikundi cha Palestina cha Hamas.

Israel imeapa ‘kuivunja kabisa Hamas’ wakati wanajeshi wake wakikusanyika katika mpaka wa Gaza.

Pia wakati kivuko kinachodhibitiwa na Misri kuingia kwenye eneo hilo kikitarajiwa kufunguliwa tena kumekuwa na juhudi za kidiplomasia za kufikisha misaada kwa mamilioni ya Wapalestina waliozingirwa huko baada ya mashambulizi mabaya ya Hamas katika miji ya mpakani ya Israel.

Maafisa wa juu wa Marekani wameonya kuwa vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas vinaweza kuenea zaidi.

Wakati huo huo meli za kivita za Marekani zikiwa zinaelekea katika eneo huku ikiripotiwa mapigano yameongezeka kwenye mpaka kaskazini mwa Israel na Lebanon.

Maelfu ya Wapalestina wameondoka Gaza City kuelekea kusini mwa eneo hilo baada ya Israel kuwaamrisha kufanya hivyo. Lakini Hamas imewataka wasiende popote.

Wapalestina baadhi yao wakiwa na pasipoti za kigeni wakitarajiwa kuvuka kuingia Misri, huku wengine wakisubiri misaada iletwe Ukanda wa Gaza, October 16, 2023.
Wapalestina baadhi yao wakiwa na pasipoti za kigeni wakitarajiwa kuvuka kuingia Misri, huku wengine wakisubiri misaada iletwe Ukanda wa Gaza, October 16, 2023.

Wapalestina wanataabika kutafuta sehemu salama za kujificha, lakini Hamas imewaonya watu wasiondoke kwenye nyumba zao, ikisema kuwa darzeni za watu wameuwawa na mashambulizi yaliyofanywa kwenye magari, na magari makubwa yaliyobeba wakimbizi, ambapo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha taarifa hii.

Forum

XS
SM
MD
LG