Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 14, 2024 Local time: 14:03

Burkina Faso imekanusha ripoti ya HRW kuhusu mauaji yaliyofanywa na wanajeshi


Ramani ya Burkina Faso ikionyesha baadhi ya miji nchini humo.
Ramani ya Burkina Faso ikionyesha baadhi ya miji nchini humo.

HRW imeyataja mauaji hayo miongoni mwa matukio mabaya ya unyanyasaji unaofanywa na jeshi la Burkina Faso tangu 2015

Burkina Faso inayotawaliwa na jeshi imekanusha ‘shutuma zisizo na msingi’, za ripoti ya Human Rights Watch-HRW kwamba wanajeshi waliwaua wana vijiji wasiopungua 223 katika mashambulizi mawili ya Februari 25.

“Serikali ya Burkina Faso inapinga vikali na kulaani shutuma hizo zisizo na msingi”, waziri wa mawasiliano Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo alisema katika taarifa yake Jumamosi jioni. “Mauaji ya Nodin na Soro yalipelekea kufunguliwa kwa uchunguzi wa kisheria”, alisema.

Waziri huyo alielezea kushangazwa kwake kwamba wakati uchunguzi huu unaendelea ili kubaini ukweli na kuwatambua waandishi, HRW imeweza, kwa fikra zisizo na mpaka, kutambua “wahalifu” na kutangaza hukumu yake.

HRW imeyataja mauaji hayo kuwa miongoni mwa matukio mabaya zaidi ya unyanyasaji unaofanywa na jeshi nchini Burkina Faso tangu mwaka 2015.

Forum

XS
SM
MD
LG