Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 30, 2024 Local time: 00:17

Boti ya uvuvi imezama katika mto Zambezi na kuua watu


Ajali ya boti ya uvuvi nchini Msumbiji
Ajali ya boti ya uvuvi nchini Msumbiji

Boti ilikuwa imebeba jumla ya watu 12 wengi wao wakiwa wakulima msimamizi wa wilaya ya Caia aliliambia shirika la habari la AFP.

Boti ya uvuvi ilizama katika mto Zambezi katikati mwa Msumbiji na kuua watu wanane wakiwemo watoto sita, mamlaka imesema Jumanne.

Kuzama kwa boti siku ya Jumatatu katika jimbo la Sofala kumetokea wiki moja baada ya ajali ya meli kuuwa watu 100 wengi wao wakiwa watoto, karibu kilomita 1,000 kuelekea kaskazini zaidi.

Boti hiyo ilikuwa imebeba jumla ya watu 12, wengi wao wakiwa wakulima, Nobre dos Santos, msimamizi wa wilaya ya Caia aliliambia shirika la habari la AFP.

Watu wawili walinusurika na wengine wawili bado hawajulikani waliko, alisema na kuongeza kuwa sita kati ya waliofariki walikuwa watoto.

Maafisa wanasema kuwa utafutaji unaendelea kwa ajili ya kuwaokoa watu hao waliopotea.

Hapo Aprili 7, boti iliyotengenezwa kienyeji iliyokuwa imebeba mizigo ilipinduka na kuua watu 98. Ilikuwa imebeba familia nyingi zilizojaa hofu wakijaribu kukimbia mlipuko wa kipindupindu ulioenea katika eneo.

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani, imerekodi karibu visa 15,000 vya ugonjwa wa kipindupindu na vifo 32 tangu mwezi Oktoba, kulingana na takwimu za serikali.

Forum

XS
SM
MD
LG