Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 04:18

Wimbo wa Beatles wanadiwa kwa dola milioni 1.2


Kundi la Beatles likipungia wapenzi wa muziki baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kennedy, New York mwaka 1964.
Kundi la Beatles likipungia wapenzi wa muziki baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kennedy, New York mwaka 1964.

Maandishi ya wimbo mmoja wa kundi maarufu la zamani la Beatles umenunuliwa katika mnada wa New York kwa dolla milioni 1.2.

Maandishi ya mkono ya wimbo ulioimbwa na kundi maarufu la zamani katika muziki wa rock ' n roll la Uingereza, Beatles, yameuzwa katika mnada mmoja wa New York Ijumaa kwa thamani ya dolla milioni moja na laki mbili, mara mbili ya kiwango kilichotazamiwa.

Wimbo huo, "A Day in the Life" uliandikwa na John Lennon katika album ya "Sgt Pepper's Lonely Hearts Club Band." Karatasi iliyoandikiwa wimbo huo kwa mkono pande zote mbili iliuzwa kwa mtu ambaye hakutajwa.

Karatasi hiyo ina maandishi yanaonyesha Lennon akirekebisha maneno ya wimbo huo kwa kalamu za rangi mbali mbali.

Wimbo huo ulipigwa marufuku na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, album hiyo ilipotolewa kwa sababu ilikuwa na maneno ya kiingereza "I'd love to turn you on" ambayo yalionekana kama fumbo katika kuunga mkono matumizi ya madawa ya kulevya.

Album hiyo ya Beatles ilipata tuzo nne za muziki za Grammy mwaka 1968.

XS
SM
MD
LG