Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:20

Wakenya wanaoishi Dubai bado wana khofu ya maisha yao


Wakenya wanaoishi Dubai bado wana khofu ya maisha yao
Wakenya wanaoishi Dubai bado wana khofu ya maisha yao

Serikali ya Dubai hivi karibuni iliweka marufuku kwa raia wa Kenya kuingia nchini humo mpaka uwe na elimu ya kiwango cha shahada. Hali hii imeleta wasi wasi kwa wakenya wanaoishi nchini humo na kusababisha khofu miongoni mwa wafanya biashara ambao kwa kawaida hununua bidhaa kutoka nchini humo.

<!-- IMAGE -->

Wafanyabiashara wengi wa Kenya husafiri kwenda Dubai kununua bidhaa kama vile magari, vifaa vya magari, vyombo vya nyumbani na hata nguo, sasa imewawia vigumu kufanya hivyo na wale waliopo Dubai wanaogopa kurudi Kenya kwani hawataweza kupata fursa ya kurudi tena nchini humo kuendelea na shughuli zao kufuatia marufuku hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Moses Wetangula amekwenda Dubai kuzungumza na kiongozi mwenzie wa nchi hiyo ili kupata suluhu ya mvutano uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Hatua ya Dubai kuweka marufuku inafuatia taarifa kwamba raia kadhaa wa nchi hiyo walihojiwa na maofisa wa uhamiaji wa Kenya na baadae kufukuzwa nchini humo.Taarifa zaidi zinasema mmoja kati ya raia hao anatoka kwenye familia ya kifalme na walikuwa nchini Kenya kwa ajili ya mapumziko.

Sauti ya Amerika-VOA imezungumza na Peterson John, raia wa Kenya anayeishi Dubai na kutaka kujua hali ikoje baada ya waziri Wetangula kufanya mazungumzo na waziri mwenzake nchini humo.

XS
SM
MD
LG