Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 17:31

Tume yapendekeza tarehe ya Uchaguzi Guinea


Tume ya taifa ya uchaguzi ya Guinea imependekeza Juni 27 kama tarehe ya uchaguzi wa rais.

Tarehe hiyo lazima iidhinishwe na serikali ya mpito inayoongozwa na Jenerali Sekouba Konate na Waziri Mkuu Jean Marie Dore.

Mtawala wa kijeshi nchini Guinea na viongozi wa upinzani walifikia makubaliano mwezi uliopita ili kurejesha utawala wa kiraia nchini humo.

Utawala wa kijeshi umekuwa ukikosolewa vikali baada ya wanajeshi kuwafyatulia risasi wapinzani katika mkutano wa hadhara mwezi Septemba na kuuwa zaidi ya watu 150.

XS
SM
MD
LG