Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 27, 2024 Local time: 02:11

Watanzania wa tofautiana juu serikali ya mseto zanzibar


Baadhi ya wanachama wa chama cha upinzani cha CUF na wale wa chama cha CCM jijini Dar-Es Salaam, wametoa maoni tofauti kuhusiana na mtazamo wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar kama suluhisho la kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

Baada ya Baraza la wawakilishi kuridhia hoja ya kutaka kuwepo serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo kinachosubiriwa kwa sasa ni kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupeleka muswada katika baraza hilo na kufanyika kwa kura ya maoni itakayosimamiwa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Katika mahojiano maalumu jijini Dae-Es Salaam kwenye ofisi ndogo ya makao makuu ya C.C.M, Lumumba baadhi ya wanachama wa chama hicho akiwemo katibu wa CCM mkoani humo Kirum Mbeng’enda, walionesha kuunga mkono wazo la kuwepo serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.

Hata hivyo mwanachama Ali Msuko alikuwa na mtazamo tofauti na kuhoji kwa nini CUF wakubali maridhiano hivi sasa. “Maslahi ya wa-Zanzibar yamewekwa kama bango lakini ni kuwatafutia watu vyeo, watu kula, kwa nini hao wanaotaka maslahi ya Zanzibar wasikanye upinzani wakaitetea Zanzibar tukawaona na tukawasikia si wamo kwenye baraza la wawakilishi na wako kwenye upinzani waikosoe serikali nah ii ndio maana ya mfumo wa vyama vingi sasa sasa inaonekana walikubali vyama vingi wakadhani vyama vingi vitawapeleka madarakani sasa uchaguzi umefanyika mara tatu hawajaingia madarakati sasa wamechoka na uchaguzi wanaona ni afadhali waingie madarakani kwa njia ya serikali shirikishi”.

Kwa upande wao wanachama wa CUF waliohojiwa kwenye makao makuu ya chama hicho huko Buguruni wengi walionesha kuunga mkono serikali ya mseto, hata hivyo hawakusita kutia shaka juu ya utekelezaji wake kulingana na yaliyotokea kipindi cha nyuma.

XS
SM
MD
LG