Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 14:01

Marekani yajaribu kuondoa mvutano Copenhagen


Marekani inaahidi kusaidia kuchangisha dola bilioni 100 kwa mwaka kwa ajili ya nchi maskini kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, hatua ambayo inaweza kusaidia mazungumzo kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa huko Copenhagen.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alitoa matamshi hayo baada ya kuwasili kwenye mkutano Alhamisi, ambapo maafisa wengi wa vyeo vya juu walielezea wasiwasi iwapo mazungumzo yatakuwa na matokeo yenye muafaka.

Clinton anasema kupatikana kwa fedha hizo kunategemea uwezo wa maafisa kufikia juhudi mbadala ambazo zinajumuisha mataifa yote makubwa. Lakini pia alionya Marekani haitatia saini mkataba wowote wa kupunguza hewa chafu kama hakuna uwazi.

Marekani inasema nchi zote lazima zikubaliane na baadhi ya kanuni, lakini China inapinga madai hayo. Akizungumza huko Beijing, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Jiang Yu, alizitaka nchi zinazoendelea kuonyesha mfano bora, pale inapotokea kusaidia nchi maskini kupunguza utowaji wa hewa chafu.

XS
SM
MD
LG