Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 13:05

Annan awashtusha viongozi wa Kenya


Serikali ya Kenya jana ili kua katika hali ya mtaharuku baada ya katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan bila ya kutarajiwa kuwasilisha majina ya wanaodhaniwa walihusika na ghasia baada ya uchaguzi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko The Hague.

Mkutano na waandishi habari ulopangwa awali na serikali uliahirishwa wakati ujumbe wa Kenya unaohusika na mashauriano na bwana Annan na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kua na mikutano ya dharura na rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga.

Baadaye serikali ilitoa taarifa iliyothibitisha kuwa bwana Kibaki na bwana Odinga walipewa taarifa rasmi kuhusu uamuzi wa bwana Annan na kueleza nia ya Kenya kutekeleza kanuni walizokubaliana na mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Louis Moreno-Ocampo.

Orodha ya wanaoshukiwa ilihifadhiwa chini ya uangalizi wa katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa wakati Kenya inachunguza uwezo wa kuwashitaki ndani ya nchi hiyo.

Ujumbe wa mawaziri wa Kenya ulikua na mkutano wa dharura wiki iliyopita na bwana Annan na bwana Ocampo baada ya kugundulika kuwa Kenya haiwezi kufikia mwezi wa mwisho ulipangwa wa augusti wa kuunda mahakama ya uhalifu ndani ya nchi.

Taarifa kutoka kwa bwana Annan ilisisitiza hatua yake ya jana inafuatana na majadiliano yaliyofanyika pamoja na ujumbe wa Kenya. Lakini wajumbe wa Kenya hapo awali walisema kwamba walikubaliana kuwa Kenya imepewa mpaka mwezi septemba na ikiwezekana mpaka julai 2010, kutafuta suluhisho la ndani kabla ya majina kuwakilishwa katika mahakama ya ICC.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG