Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 13, 2024 Local time: 02:32

Mahakama nchini Mali imetangaza haina uwezo kuchunguza kesi za kijeshi


Ramani ya Mali na maeneo jirani na nchi hiyo.
Ramani ya Mali na maeneo jirani na nchi hiyo.

Mahakama ilitoa uamuzi kutoruhusiwa ombi kutoka kwa vyama vya mahakimu kuiona kuwa Mali ilikuwa na  mapungufu  ya kisheria

Mahakama ya Katiba nchini Mali imejitangaza yenyewe kuwa haina uwezo kuchunguza kesi inayotaka utawala wa kijeshi kusitisha shughuli za vyama vya kisiasa kubatilishwa.

Katika waraka ulioonekana na shirika la habari la AFP leo Jumamosi, mahakama hiyo pia ilitoa uamuzi wa kutoruhusiwa ombi kutoka kwa vyama vya mahakimu na waendesha mashtaka, kuiona kuwa Mali ilikuwa na mapungufu ya kisheria au mwanya wa kitaasisi na kupanga mchakato wa kurejea katika uchaguzi. Hukumu zote mbili za mahakama zilitolewa siku ya Alhamisi.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limetawaliwa na serikali ya kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021, huku hali ya usalama ikizidi kuzorota kutokana na makundi ya wanajihadi na wanaotaka kujitenga.

Forum

XS
SM
MD
LG