Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 30, 2024 Local time: 06:24

Wafadhili waahidi dola milioni 629 kwa Ethiopia kukabiliana na mzozo wa kibinadamu


COP28 Climate Summit
COP28 Climate Summit

Mkutano wa ngazi ya juu wa kuahidi misaada kwa Ethiopia, uliofadhiliwa na Ethiopia, Uingereza, na Umoja wa Mataifa ulipokea karibu dola milioni 628.9 kama msaada wa kibinadamu wa kuokoa maisha kwa mamilioni ya raia wa nchi hiyo wanaoteseka.

Idadi kubwa ya Waethiopia wamekuwa wakikabiliwa na athari mbaya za migogoro, ikiwa ni pamoja na na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ethioia ilitaka kiasi cha dola bilioni moja.

"Tunaelewa huu ni mwanzo tu, na tunatumai kuendelea kuongezeka kwa uungwaji mkono kwa mwaka mzima," alisema Joyce Msuya, msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu.

Kati ya nchi 21 zilizoshiriki, Marekani ndiyo ilikuwa mfadhili mkubwa zaidi kwa kuahidi dola milioni 154, ikifuatiwa na Uingereza, dola milioni 124.58 na Umoja wa Ulaya, dola milioni 139.

Mpango wa mwezi uliopita wa kutafuta mabilioni ya dola, ya misaada ya kibinadamu, kufikia sasa umepata ufadhili wa chini ya asilimia 5, kiasi ambacho hakitoshi kushughulikia mahitaji makubwa ya watu milioni 15.5, wanaokabiliwa na migogoro na majanga ya hali ya hewa yanayofuatana moja baada ya jingine.

Forum

XS
SM
MD
LG