Zaidi ya mahujaji milioni 2.5 kuanza ibada ya Hijja Ijumaa

Mahujaji wakizunguka jengo la Kaaba katika msikiti mtukufu wa Makka, Saudi Arabia  ikiwa ni sehemu ya ibada ya Hijja.

Kikosi maalum cha jeshi la miamvuli la Saudi Arabia wakijitayarisha na shughuli za usalama kwa ajili ya tukio la Ibada ya Hijja wakiwa katika mji mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia, Sunday, Agosti. 4, 2019.

Polisi wa Saudi Arabia akiangalia harakati zinazoendelea katika msikiti wa Makka kwa kutumia katika Kompyuta ambayo imeunganishwa na kamera zilizowekwa ndani ya msikiti huo,.Saudi Arabia, Jumanne, Agosti. 6, 2019.

Mchoraji Eid Al Salwaawi akimaliza kuchora picha ya Kaaba na maeneo mengine ya ibada ya Hijja, Mecca, Cairo, Misri, Julai 17, 2019.

Mahujaji wakigusa mlango wa dhahabu wa jengo la pembe nne la Kaaba katika msikiti mtukufu wa Makka, Agosti 07, 2019, kabla ya ibada ya Hijja.(AP Photo/Amr Nabil)

Hujaji akifunika kichwa chake kujizuia na joto lililoripotiwa kuongezeka kufikia nyuzi joto 42 katika msitiki mtukufu wa Makka nchini Saudi Arabia.

Mahujaji wakigusa mlango wa dhahabu wa jengo la kaaba.

Zaidi ya mahujaji milioni 2.5 wataanza ibada ya kila mwaka ya Hijja siku ya Ijumaa katika mji mtukufu wa Makka, Saudi Arabia, wakati mgogoro ukiwa unaendelea katika Ghuba. Makundi ya mahujaji wameanza kukusanyika katika mji wa Makka siku chache kabla ya Hijja, ikiwa ni tukio muhimu la mwaka wa Kiislam.