Shambulizi la 'kigaidi' laua watu 40 Niger

Wanakijiji wakusanyika katika eneo la shambulizi katika kijiji cha Solhan, katika mkoani wa Yagha kwenye mpaka wa Niger, Burkina Faso Prime Minister's Press Service/Handout via REUTERS.

Raia watano, wanajeshi wanne na washambuliaji 40 wenye silaha waliuawa Jumapili wakati mapigano katika mkoa uliyokuwa na ghasia wa Niger, kusini magharibi, karibu na mpaka na Mali, serikali imesema.

Karibu magaidi wenye silaha nzito 100 wanaoendesha pikipiki walikishambulia kijiji cha Tchoma Bangou, kiasi cha majira ya saa tisa alfajiri.

Kwa mujibu wa AFP siku ya Jumapili, Wizara ya Ulinzi ya Niger ilisema katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya umma bado hawajawatambua wale waliohusika na tukio hilo baya la hivi karibuni.

Mwitikio wa haraka na wa nguvu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama uliwezesha kuzuia shambulio hilo na kusababisha hasara kubwa kwa adui, wizara ilisema, na kuongeza kuwa wanajeshi wake walikuwa wamekamata pikipiki na silaha kadhaa, pamoja na AK47 na bunduki za rashasha kutoka kwa washambuliaji.

Tchoma Bangou iko katika mkoa wa Tillaberi, unaopakana na Mali na Burkina Faso, eneo linalojulikana kama mipaka mitatu ambayo imekuwa ikilengwa mara kwa mara na vikundi vya kijihadi.