Mkuu wa jeshi wa Ukraine ametoa ripoti hiyo kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wa Facebook. Kando la hilo ripoti zimeongeza kusema kwamba Russia imepoteza wanajeshi 819 katika siku moja iliyopita, ingawa Russia hajajibu madai hayo.
Jeshi la wanahewa la Ukraine limesema Jumapili kwamba vikosi vyake vimeangusha droni 16 kati ya 18 zilizorushwa na Russia dhidi ya maeneo tofauti ya Ukraine. Jumamosi wakati wa maadhimisho ya miaka 2 tangu kuanza kwa uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine, rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy alishukuru wote ambao wamekuwa wakisasidia taifa lake.
“Kutokana na usaidizi wao, mamilioni ya watu wa Ukraine pamoja na majirani wao wanaozunguka Russia, wanajihisi kuwa nchi zao haziwezi kuwa eneo la Putin,” amesema Zelenskyy.