Matayarisho ya sherehe za miaka 243 ya kuzaliwa kwa taifa la Marekani

Moja ya magari ya kivita aina ya Bradley Fighting Vehicles likiendeshwa kuingia katika uwanja wa Kumbukumbu wa Lincoln Memorial kwa ajili ya matayarisho ya salamu za Rais wa Marekani Donald Trump kwa taifa siku ya uhuru wa Marekani Julai 4, 2019, Washington.

Gari jingine la kivita aina ya Bradley Fighting Vehicles

the Lincoln Memorial fMatayarisho ya siku ya uhuru ya Marekani yakiendelea mjini Washington katika uwanja wa Lincoln Memorial.

Gari za kivita zikiwa tayari kutoa ulinzi wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa Marekani Alhamisi.

Mmoja wageni wanaotembelea Washington katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Marekani akijaribu kuvuka vizuizi.

Vyoo vilivyokuwa katika eneo la maadhimisho

Wageni wakiwa katika eneo wakati wa maandalizi ya siku ya Uhuru wa Marekani.

Mwanajeshi wa majini wakitengo cha ufundi wa elektroniki Samuel McIntire, mbele kulia na wengine wakifanya mazoezi kabla ya sherehe mbele ya gari la kivita.

Rais Donald Trump atatoa hotuba ya salamu zake kwa taifa la Marekani Alhamisi, Jioni