Macron kupambana na Le Pen katika duru ya pili ya uchaguzi Ufaransa

Your browser doesn’t support HTML5

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameanza kampeni kali ya wiki mbili kabla ya duru ya pili ya uchaguzi April 14, ambapo anakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Marine Le Pen mgombea wa siasa kali za mrengo wa kulia.
Rais Macron alipata asilimia 27.85 za kura wakati wa uchaguzi wa rais siku ya Jumapili akifuatiwa na Bi. Le Pen, kiongozi mwenye siasa kali za kulia aliyepata asili mia 23.15.
Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Paris, Mohamed Saleh mchambuzi wa masuala ya kisiasa, anasema kuna wasi wasi kwamba huwenda Le Pen akapata ushindi ikiwa baadhi ya wafuasi wa Jean-Luc Melenchon wa mrengo wa kushoto watampigia kura.