Kenya itaanza kutengeneza chanjo ya COVID-19 2022

Your browser doesn’t support HTML5

Kenya yajipanga kutengeneza chanjo ya COVID-19

Mwaka 2022 Kenya itaanza kutengeneza chanjo ya COVID-19 ndani ya nchi kwa kushirikiana na kampuni za dawa katika hatua ya kurahisisha usambazaji wa chanjo kwa watu wengi.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitoa muongozo wa utengenezaji wa chanjo ya ndani, kwamba Kenya imeanza mchakato wa kujenga mtambo wa kujaza chanjo za COVID-19.

Kiwanda kamili cha kutengeneza chanjo kitajengwa mwaka 2024 alisema Kagwe.

Kiwanda hicho kitasaidia nchi hiyo kujaza chanjo zake kutoka kwa wazalishaji wakuu kwenye vichupa au sindano, kuzifunga na kuzipanga kwa ajili ya usambazaji.

Watengenezaji wengi wa chanjo wanatumia watu wengine kujaza na kumalizia ufungaji wa chanjo zao na nchi za kiafrika kama Senegal, Rwanda, na Afrika Kusini zipo katika mazungumzo na wawekezaji kuanza uzalishaji wa chanjo ya virusi vya corona.

Hata hivyo Kenya itahitaji kuhakikisha inapata ushirikiano na mmiliki mwenye hati ya chanjo ili kutengeneza chanjo hiyo.