Amnesty, HRW zaishutumu Tanzania kwa ukandamizaji

Rais John Magufuli

Mashirika yanayotetea haki za binadamu, Amnesty International na Human Rights Watch yanaishutumu serikali ya Tanzania kwa kukandamiza vyombo vya habari, mashirika yasiokuwa za serikali na hata wanasiasa nchini humo.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Amnesty, Human Rights Watch

Katika ripoti yao mpya iliyotolewa leo mjini Nairobi mashirika hayo yanasema yamefikia hitimisho hilo baada ya mahojiano na Waandishi wa habari 80, waandishi wa blogi, wanasheria, wawakilishi wa asasi zisizo za kiserikali, wanachama wa vyama vya siasa na hata maafisa wa serikali ya Tanzania.

Kauli zao zimedhihirisha jinsi serikali ya Rais John Magufuli inavyonyanyasa waandishi wa habari na wanasiasa ambao walikuwa wanatekeleza haki yao ya uhuru wa kujieleza na kushiriki katika harakati za siasa nchini humo. Ripoti hiyo imeeleza kuwa ukadamizaji huo ulianza tangu mwaka 2015.

Akizungumza na waandisha wa habari wakati wa kuzinduliwa kwa ripoti hiyo, mtafiti wa shirika la la kimataifa la Amnesty Ronald Ebole , amesema Ripoti hizo zinaonyesha jinsi mamlaka za Tanzania zilivyokiuka haki ya uhuru wa kujieleza, uhuru wa kushirikiana na uhuru wa vyombo vya habari.

Ripoti aidha inaeleza jinsi serikali ilivyofunga baadhi ya vyombo vya habari kwa kuandika maudhui yaliyonekana kukosoa serikali.

“Mwezi Julai Magufuli alipiga marufu shughuli za kisiasa na wanasiasa kadha wa upianzani wakakamtwa na kushtakiwa . Mbunge wa Kigoma Mjini nchini Tanzania Zitto Kabwe anaelezea kuwa taifa la Tanzania linapitia wakati mgumu sana kuhusiana na masuala ya haki za binadamu.

Ripoti hiyo pia inaeleza Sera na Matukio kadamizi yanayodaiwa kunyamazisha vyombo vya habari na kuzidisha hofu kwa wenye kupaza sauti hasa tangu kukamatwa kwa mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Erick Kabendera.

Zitto aidha anasema dunia haipaswi kunyamza visa vya dhulma vikiendelea nchini tanznai

Ikiwa bado ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa tanznia ,Mashirika ya Amnesty na human rights watch yanaitaka serikali kuonyesha nia ya kulinda uhuru wa kujieleza kama inavyolindwa katika katiba.

Imetayrishwa na mwandishi wetu, Hubbah Abdi, Kenya.