Wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga, wameitisha maandamano kulalamikia kile wamedai kama kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini Kenya na utawala mbovu. Rais William Ruto ametishia kukabiliana na waandamanaji kwa nguvu zote. Ruto, ametoa wito kwa Odinga kufanya mazungumzo na serikali kwa kuheshimu sheria zilizopo na wala sio kutumia maandamano ambayo mara nyingi huambatana na vifo na uharibifu wa mali
MANDAMANO YA UPINZANI KENYA YAMEKOSA JOTO.mp3
Your browser doesn’t support HTML5
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga alishindwa kuongoza wafuasi wake kwa maandamano kuingia katikati mwa jiji la Nairobi baada ya maafisa wa usalama kushika doria.
Kennes Bwire amezungumza na mchambuzi wa siasa Prof Harman Manyora