Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:01

Zimbabwe yaruhusiwa kuuza almasi zake nje .


Wachimba almasi wakifanya kazi yao katika mgodi wa Marange.
Wachimba almasi wakifanya kazi yao katika mgodi wa Marange.

Zimbabwe yaruhusiwa kuuza almasi zake nje baada ya mkutano na Kimberly process huko Kinshasa.

Zimbabwe imefikia makubaliano ya kuuza almasi zake zilizochimbwa katika mgodi wenye mzozo wa Marange.

Baraza la almasi duniani lilisema makubaliano hayo yalifikiwa jumanne kwenye mkutano katika mji mkuu wa Congo Kinshasa. Iliidhinishwa na wanachama wa Kimberly Process mpango uliowekwa kuzuia kile kilichoitwa almasi za damu kufikia masoko ya kimataifa .

Makubaliano hayo yanaruhusu migodi miwili ya Marange kuuza almasi kwenye soko la kimataifa. Mgodi wa tatu ulioendeshwa na kampuni ya wachina ya Angin , utaruhusiwa kuanza tena mauzo kufuatia kupitishwa na wasimamizi wa Kimberly.

XS
SM
MD
LG