Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:32

Zimbabwe yapunguza idadi ya wafanyakazi wa serikali ofisini kutokana na Covid


Sehemu ya mji wa Harare, Zimbabwe ikuwa na watu wachache kutokana na kufungwa kwa shuguli za kawaida kwa ajili ya Covid.
Sehemu ya mji wa Harare, Zimbabwe ikuwa na watu wachache kutokana na kufungwa kwa shuguli za kawaida kwa ajili ya Covid.

Huduma za serikali nchini Zimbabwe zimeathiriwa pakubwa baada ya amri ya kufunga baadhi ya shuguli za kawaida ili kupunguza mambukizi ya virusi vya corona wakati idadi ya vifo iliongezeka nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, taifa hilo la kusini mwa Afrika limefungiwa shuguli za kawaida tangu Januari, wakati wiki iliopita serikali ikitoa amri kwamba asilimia 10 pekee ya wafanyakazi wa serikali wawe ofisini ili kuzuia maambukizi.

Janga hilo limeathiri maafisa wa ngazi za juu serikalini ambapo tayari mawaziri wanne wamekufa, watatu miongoni mwao wakifa katika kipindi cha wiki mbili zilizopota. Ofisi nyingi za serikali zilionekana tupu kuanzia Jumatatu, wakati maafisa wa dharura pekee wakibaki.

Kwenye ofisi za kutoa pasi za kusafiria, huduma za dharura zinatolewa pekee kwa wale wanaoonyesha vibali vya kufanya kazi kwenye mataifa ya nje. Kwenye ofisi ya wizara ya elimu, ni maafisa wa mitihani pekee waliobaki.

Zimbabwe yenye jumla idadi ya watu milioni 15 kufikia sasa imeshuhudia maambukizi 31,320 na vifo zaidi ya 1,000. Kuna wasi wasi kuwa huenda watu wa Zimbabwe wanaoishi Afrika kusini waliingia nchini na aina mpya ya virusi vya Covid, wakati wa kipindi cha siku kuu za mwisho wa mwaka.

Mtayarishi- Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG