Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 08:03

Zimbabwe: Wafanyakazi wa afya hawaruhusiwi tena kufanya mgomo wa muda mrefu


Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

Zimbabwe imepiga marufuku wafanyakazi wa afya kufanya mgomo wa muda mrefu, huku walioandaa mgomo wakikabiliwa na kifungo kwa mujibu wa sheria mpya iliyotangazwa Jumanne ambayo inaelezewa na makundi ya kutetea haki za binadamu kama “kandamizi”.

Wawakilishi wa wafanyakazi ambao wanaitisha au kuandaa maandamano kwa kukiuka sheria hiyo wanakabiliwa na kifungo cha hadi miezi sita jela na kulipa faini, chini ya sheria hiyo.

Wafanyakazi walioshiriki katika mgomo wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Chama cha madaktari wa Zimbabwe kwa ajili ya haki za binadamu (ZADHR) kimesema sheria hiyo inaweza kupelekea wafanyakazi zaidi kutafuta ajira nje ya nchi.

“Mswaada huu hakika ni kandamizi,” mkurungenzi wa ZADHR ameiambia AFP.

Madaktari na wauguzi wengi walihamia nje ya nchi katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya mazingira mabaya ya kazi na malipo duni kufuatia mfumuko mkubwa sana wa bei.

XS
SM
MD
LG