Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 03:39

Zimbabwe kupiga kura juu ya katiba mpya


Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai
Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai

Wanaharakati wa kidemokrasia wanapinga tarehe ya kura ya maoni na wametishia kupeleka malalamiko yao mahakamani.

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai anasema nchi hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa bunge na urais mwezi Julai baada ya kupiga kura maoni juu ya katiba mpya mwezi Machi.

Alisema hayo Jumatano baada ya waziri wa maswala ya katiba Eric Matunenga kupanga tarehe ya Machi 16 kwa ajili ya kupiga kura ya maoni.

Katika mkutano na waandishi wa habari huko Harare , Matinenga alieleza wasi wasi wake kuwa muda hautoshi na pengine muda zaidi huenda ukahitajika kwa ajili ya uchaguzi wa Machi.

Baraza la kitaifa la bunge (NCA) ambalo linajumiwsha makundi ya harakati za kidemokrasia huko Zimbabwe limesema litapinga tarehe upigaji kura wa maoni hapo Machi 16 mahakamani .

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika mwenyekiti NCA Lovemore Madhuku amesema kundi lake linataka serikali itoe kipindi cha mdahalo cha miezi miwili hivi kabla ya wapiga kura kufanya uamuzi wao juu ya katiba mpya.

Chama cha Bw. Tsvangirai cha MDC na kile cha rais Robert Mugabe cha ZANU PF wote wanaunga mkono mabadiliko hayo mapya.
Jumuiya ya maendeleo ya Afrika Kusini inataka katiba mpya iidhinishwe kabla ya Zimbabwe kufanya uchaguzi mkuu.
XS
SM
MD
LG