Zimbabwe ilianza mfululizo wa uchaguzi mdogo leo Jumamosi huku upinzani ukiwa katika hali ya taharuki baada ya kutengwa katika orodha ya wapiga kura.
Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe imesema kupitia mtandao wa X zamani ukiitwa Twitter, kwamba vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za huko, bila kutoa maelezo zaidi.
Uchaguzi mdogo wa maeneo tisa ulitarajiwa kufanyika lakini wagombea wengi wa upinzani waliondolewa kwenye orodha ya uchaguzi na mahakama, katika kipindi cha ghasia za uchaguzi.
Wakazi walisema hakuna upigaji kura uliofanyika katika wilaya ya Harare ambako moja ya uchaguzi mdogo ulipangwa kwa sababu mgombea wa chama tawala cha ZANU-PF amepita bil yaa kupingwa.
Uchaguzi wa nchi nzima uliofanyika mwezi Agosti ulishuhudia Rais Emmerson Mnangagwa, akiingia muhula mpya na chama chake cha ZANU-PF ambacho kilipata viti 177 kati ya 280 vya bunge la taifa, huku chama cha upinzani cha Citizens Coalition for Change kikichukua viti 104.
Forum