Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 06:06

Umoja wa mataifa watoa wito wa msaada zaidi kuokowa maisha Zimbabawe


mkazi wa kijiji cha Nsezi, Matabeleland, Zimbabwe.
mkazi wa kijiji cha Nsezi, Matabeleland, Zimbabwe.

Watu wataathiriwa vibaya na upungufu wa chakula na wengi hawatoweza kutegemea mifugo yao, kwa vile maelfu ya mifugo imekufa kutokana na ukosefu wa maji na ardhi ya malisho.

Umoja wa mataifa unasema takriban watu millioni 3 waliokumbwa na ukame nchini Zimbaawe watakabiliwa na njaa. Umoja wa mataifa unatarajia idadi hiyo ikaongezeka hadi watu millioni 4 pale mfumo wa hali ya hewa wa El Nino utakapoingia.

Mratibu mkazi wa umoja mataifa kwa Zimababwe Bishow Parajuli, anasema atahri ya mvua chache na mavuno duni kufwatia miaka 2 ya ukame zinaonekana wazi huko Matabeleland na maeneo mengine makavu.

Bw Parajulli anasema kuwa alitembelea eneo hilo na baadhi ya wafadhili na mabalozi. Tumeona hali jinsi ilivyo mbaya sana

Wiki kadhaa zilopita umoja mataifa ulitoa ombi la dola millioni 360 ili kutoa msaada wa kuokowa maisha kwa zaidi ya watu millioni 3. Mahitaji yanayopewa kipaumbele ni kwa chakula, maji, afya, lishe, usafi wa vyoo na hifadhi.

Parajuli anasema dola millioni 70 zimepokelewa, na kuacha pengo la dola millioni 290. Anasema ni muhimu kwa wafadhili kujibu kwa ukarimu na kwa haraka wito ombi hilo.

Bw Parajuli anasema, kwa vile Zimbabwe ni taifa lisilo na bahari, na kadhalika eneo zima la kusini mwa Afrika limeathiriwa na El Nino, kadhalika ukosefu wa mahindi ya ziada, ni muhimu sana kufanya mipango ya mapema katika misingi ya uagizaji kutoka nje na mfumo wa ugavi. Kwa hivyo majibi ya mapema kwa msaada yatasaidia kuokowa maisha na mateso miongoni mwa raia.

Parajuli anasema anawasiwasi mkubwa kuhusu kipindi hiki cha mavuno hafifu kati ya September na Marchi. Hiki ni kipindi cha baina ya mavuno pale akiba ya chakula ya wakulima huwa imepungua.

Anasema watu wataathiriwa vibaya na upungufu wa chakula na wengi hawatoweza kutegemea mifugo yao, kwa vile maelfu ya mifugo imekufa kutokana nan a ukosefu wa maji na ardhi ya malisho.

XS
SM
MD
LG