Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:04

Angola yatangaza kuwepo wagonjwa wawili wa Zika


FMbu Aedes anayebeba kirusi cha Zika. Jan. 27, 2016.
FMbu Aedes anayebeba kirusi cha Zika. Jan. 27, 2016.

Kujitokeza kwa ugonjwa wa Zika Afrika litakuwa ni jambo la wasiwasi mkubwa kwa sababu ya hali duni ya miundo mbinu ya afya ya jamii katika nchi nyingi, ikiwemo Angola

Angola imetangaza kuwa ina wagonjwa wawili wenye virusi vya Zika, lakini haijaeleweka iwapo aina yake ndiyo ile ambayo inaeneza ugonjwa huo huko katika bara la Amerika.

Shirika la habari la Ureno, Lusa limesema moja ya wagonjwa hao ni Mfaransa. Mgonjwa mwengine amepatikana katika manispaaa ya Viana kwenye jimbo la Luanda. Wote wawili wamesajiliwa katika wiki za karibuni.

Hakuna kirusi cha Zika kilichosababisha kuenea kwa ugonjwa huo nchini Brazil na maeneo mengine kimeripotiwa kuathiri katika bara la Afrika, japokuwa shirika la afya duniani (WHO) mwezi Mei lilitangaza kuwa kirusi hicho kiliwaathiri watu wa Cape Verde, ambacho ni kisiwa kilichoko mbali na pwani ya Afrika Magharibi.

Kujitokeza kwa ugonjwa huu Afrika litakuwa ni jambo la wasiwasi mkubwa kwa sababu ya hali duni ya miundo mbinu ya afya ya jamii katika nchi nyingi, ikiwemo Angola. Wakati nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inashindana na Nigeria kuwa na jina la nchi inayozalisha petroli kwa wingi, ilhali ikiwa ni moja ya nchi maskini sana duniani.

Historia ya nchi hii iliyokuwa koloni la Ureno, ilikabiliwa na mlipuko wa homa ya manjano kwa miaka kumi, na hivi karibuni ilikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu.

Zika kimsingi ni ugonjwa unaoenezwa na mbu. Mnamo mwezi Novemba, Shirika la afya duniani iliondoa ilani yake ya mwezi moja ikitahadharisha juu ya kirusi hiki kwa afya ya jamii akisema hili janga linaweza kuendelea.

XS
SM
MD
LG