Hivi sasa njaa kubwa inatishia taifa hilo kufuatia ukame ambao tayari umeuwa watu 43,000 mwaka 2023.
Wananchi milioni 8.3 wa Somalia karibu nusu ya watu wote katika nchi hiyo, wana shida kubwa ya msaada wa kibinadamu, amesema Guterres akiongeza kuwa ni asilimia 15 tu ya msaada wa dola bilioni 2.6 zilizohitajika kwa nchi hiyo ambayo imefikiwa.
Alikuwa akizungumza baada ya kutembelea kambi ya Baidoa , kusini magharibi mwa somalia , kwa watu waliokoseshwa makazi kutokana na ukame na mapigano baina ya kundi la al shabaab lenye uhusiano na al qaida na vikosi vya serikali.
Baada ya vipindi vitano mfululizo vya mvua kushindwa ukame umewakosesha makazi wasomali milioni 1.4 ambapo wanawake na watoto wanafikisha idadi ya asilimia 80, Alisema Guterres .
jumuiya ya usalama wa chakula IPC ambayo inaweka kiwango cha kimataifa kuamua ukubwa wa mzozo wa chakula ilisema desemba mwaka jana kwamba njaa iliepukwa kwa muda lakini ikaonya kuwa hali inazidi kuwa mbaya.