Makamu Rais wa Marekani ahimiza mageuzi Kenya
Makamu rais wa Marekani Joe Biden amesema anamatumiani uwongozi wa Kenya utatekeleza mageuzi ya siasa yanayohitajika nchini humo.
Akiwqa katika ziara ya siku tatu huko Kenya, Bw Biden aliuambia mkutano wa waandishi habari mjini Nairobi siku ya Jumanne kwamba ikiwa nchi hiyo itaidhiniusha katiba mpya na kuimarisha utawala bora, hiyo itakua nafasi kubwa ya kupokea msaada na uwekezaji kutoka Marekani.
Biden alisema hayo baada ya kukutana na rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Riala Odinga.Kuhusiana na masuala ya usalama makamu rais Biden alisema Marekani inaunga mkono juhudi za Kenya kuhakikisha usalama wa mipaka yake na Somalia, ambako wanaharakati wa kislamu wanajaribu kuipindua serekali ya mpito.
Rais Kibaki amesema Kenya imeiomba Marekani kuongoza juhudi kabambe ya kimataifa kurudisha utulivu huko Somalia.
Kenya ni kituo cha pili cha ziara ya Biden baraniu Afrika, itakayomalizikia huko Afrika ya Kusini ambako ataiwakilisha Marekani katika sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia hapo June 11.