Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:39

Zelenskyy kuhutubia baraza la Ulaya


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy .
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy .

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anahutubia mkutano wa baraza la Ulaya Jumatatu, wakati akisukuma kupatiwa misaada zaidi, na kutaka shinikizo liongezwe kwa Russia kumaliza uvamizi wake.

Rais wa baraza la Ulaya, Charles Michel amesema katika barua kabla ya mkutano huo wa siku mbili kwamba Ukraine ‘imeonyesha ushujaa kwa kweli na heshima wakati ikikabiliana na uvamizi na ukatili wa Russia." Moja ya masuala ambao yanatia wasi wasi mkubwa ni kuisaidia Ukraine, pamoja na washirika wetu wa kimataifa, kuhusu mahitaji yao ya kifedha,” amesema Michel.

"Pia tutajadili njia bora ya kutoa misaada yetu kwa Ukraine katika ujenzi mpya, kama juhudi kubwa za ulimwengu ambazo zinahitajika kuijenga tena taifa hilo." Michel amesema, akiongeza kwamba katika mikutano huenda akajumuisha suala la bei za nishati ambazo zinahusishwa na mzozo.

Mashariki mwa Ukraine, gavana wa Luhansk Serhiy Haidai. amesema Jumatatu kwamba kuna mapigano makali ya Sievierodonetsk, mji wa mwishoni unaodhibitiwa na Ukraine katika mkoa huo, huku majeshi ya Russia yakisonga mbele kwenye viunga vya mji huo.

XS
SM
MD
LG