“Lazima tujenge Vikosi vya Wanajeshi vya Ulaya ili mustakabali wa Ulaya utegemee watu wa Ulaya pekee na maamuzi kuhusu Ulaya yafanywe barani Ulaya,” Zelenskyy amesema katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Usalama wa Munich, Februari 15.
Huku kukiwa na wasiwasi mjini Kyiv na Brussels kwamba wanaweza kutengwa katika juhudi za kukomesha uvamizi kamili wa Russia, dhidi ya Ukraine, na kusababisha makubaliano ya kuipendelea Moscow, amerejea tena kwamba Ukraine na Ulaya lazima zihusishwe katika mazungumzo yoyote.
Amesema Ukraine haitakubali kamwe mikataba nyuma ya migongo inayoihusu bila kushirikishwa.
Forum