Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:26

Zelenskyy atembelea Albania


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amekuwepo Albania, Jumatano kwa mikutano na viongozi katika eneo hilo huku akitafuta uungwaji mkono zaidi katika vita vya nchi yake dhidi ya uvamizi wa Russia.

Rais Zelenskyy, amesema atajadili ulinzi na ushirikiano wa kisiasa pamoja na mpango wa amani wa Ukraine, katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Albania, Edi Rama.

“Nitapendekeza kuunga mkono juhudi za Ukraine kufikia amani ya haki na ya kudumu, pamoja na kuandaa mkutano wa kimataifa wa amani nchini Uswizi,” Zelenskyy amesema kupitia mtandao wa X.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Albania Igli Hasani alionyesha uungaji mkono kamili wa serikali yake kwa juhudi za amani za Ukraine na kujitolea kusaidia katika juhudi za ujenzi mpya nchini Ukraine.

Licha ya hayo jeshi la Ukraine, Jumatano limesema mashambulizi ya Russia yameendelea kwa kutumia ndege 10 zisizo na rubani na makombora.

Forum

XS
SM
MD
LG