Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:20

Zelenskyy aishtumu Russia kuishika Afrika mateka kwa kuzuia ngano za Ukraine


Rais wa Ukraine akiutembelea mji wa kusini wa Mykolaiv, wakati mashambulizi ya Russia yakiendelea, June 18, 2022. Picha ya Reuters
Rais wa Ukraine akiutembelea mji wa kusini wa Mykolaiv, wakati mashambulizi ya Russia yakiendelea, June 18, 2022. Picha ya Reuters

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameishtumu Russia kwa “kuishika Afrika mateka” kwa kuzuia usambazaji wa ngano na kuchangia kupanda kwa bei ya chakula katika bara hilo.

Katika hotuba kwa njia ya video kwa viongozi wa Umoja wa Afrika Jumatatu, Zelenskyy amesema, " Vita hivi vinaweza kuonekana kuwa mbali sana na kwenu na nchi zenu. Lakini kwa bahati mbaya, kupanda kwa bei ya chakula kumevifanya vita hivyo kuhisiwa na mamilioni ya familia za Afrika."

Amesema Ukraine inafanya mazungumzo magumu kwenye ngazi mbali mbali kujaribu kumaliza vikwazo vya Russia kwenye bandari za Ukraine.

"Lakini hakuna hatua iliyokwisha pigwa, ndio maana mzozo wa chakula duniani utaendelea wakati wote vita hivi vya kikoloni vinaendelea," amesema.

Russia inakanusha kuzuia kwa makusudi usafirishaji wa ngano kutoka Ukraine na kusema kupanda kwa bei ya chakula duniani ni kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa na mataifa ya magharibi dhidi ya Russia.

Mkuu wa sera ya kigeni ya Umoja wa Ulaya Joseph Borrell ametaja vitendo vya Russia kuwa "uhalifu halisi wa kivita."

Aliwambia wanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya waliokutana nchini Luxembourg Jumatatu, " Ni jambo lisiloeleweka, ni vigumu kufikiria kwamba mamilioni ya tani za ngano bado zinaziuiliwa nchini Ukraine ilihali katika sehemu nyingine ya dunia, watu wanateseka kutokana na njaa."

XS
SM
MD
LG