Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 03:26

Zelensky asema, vita vitasitishwa ikiwa Russia itaondoa wanajeshi wake nchini Ukraine


Rais Zelensky akihutubia wanajeshi wa Ukraine wakati wa ziara yake katika mji uliokombolewa wa Kherson, Novemba 14, 2022.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenseky Jumanne amesema usitishwaji wa kweli na kamili wa uhasama utatokea ikiwa Russia itaondoa wanajeshi wake wote ndani ya Ukraine na kurejesha udhibiti wa eneo la Ukraine kwenye mpaka wake na Russia.

Akihutubia viongozi wa nchi za G20 kwa njia ya mtandao kwenye mkutano mjini Bali, Zelensky amesema kuchelewesha kumaliza mzozo inamaanisha vifo zaidi vya wanainchi wa Ukraine na vitisho zaidi kwa ulimwengu.

“Ninaamini sasa ni wakati ambapo vita haribifu vya Russia vinatakiwa kukomeshwa,” Zelensky amesema.

Matamshi ya kiongozi huyo wa Ukraine yanafuatia ziara yake jana Jumatatu katika mji uliokombolewa wa Kherson ambapo aliwaambia wanajeshi wa Ukraine kwamba nchi iko tayari kwa amani.

Rais wa Marekani Joe Biden, akizungumza Jumatatu kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Indonesia, ameutaja ukombozi wa mji wa Kherson kuwa ushindi mkubwa kwa serikali ya Kyiv.

Lakini amesema washirika wa magharibi wanaoiunga mkono Ukraine hawatalazimisha suluhu kwa Ukraine kumaliza vita.

Alisema hakuna lolote litakalofanyika kuhusu Ukraine bila Ukraine kukubaliana nalo.

XS
SM
MD
LG